#Local News

KAUNTI YAONGEZA MGAO WA ELIMU YA KIUFUNDI

Serikali ya kaunti ya Trans Nzoia imeongeza mgao wa kufadhili elimu ya kiufundi kutoka shilingi milioni 7 hadi milioni 45 kila mwaka, mkurugenzi mkuu wa elimu katika serikali hiyo Eliud Luswet akisema hatua hiyo inalenga kuongeza mgao kwa kila mwanafunzi.

Kulingana na Lusweti, kila mwanafunzi katika chuo cha kiufundi atakuwa akipokea kima shilingi elfu 18 kila mwaka.

Naye mwakilishi wadin ya Kapomboi Keffa Were, amesema ufadhili huo utawahimiza vijana wengi kujiunga vyuo hivyo ili kupata ujuzi wa kujiajiri ilivyo katika mataifa yaliyoendelea.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KAUNTI YAONGEZA MGAO WA ELIMU YA KIUFUNDI

SAKATA YA MAGEREZA YAFIKISHWA MAHAKAMANI

KAUNTI YAONGEZA MGAO WA ELIMU YA KIUFUNDI

RAIS RUTO ATEUA WAZIRI 11

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *