MULILI AIGURA INGWE

Kipa Wa AFC Leopards Maxwell Mulili Ametangaza Kuachana Na Klabu Hiyo Baada Ya Miaka Mitano, Huku Ikiwa Mwaka Mmoja Kati Yake Alikuwa Kwa Mkopo Katika Klabu Ya Zoo FC Yenye Makao Yake Kericho.
Amekuwa Mwanachini Wa Levis Opiyo Kwa Miaka Michache Iliyopita Na Katika Hatua Inayoaminika Kulenga Kupata Muda Zaidi Wa Kucheza Kwengineko, Mwanafunzi Huyo Wa Zamani Wa St. Ignatius Mukumu Ameondoka Ingwe.
Aliingia Kwenye Mitandao Ya Kijamii Kutangaza Kuondoka Kwake Kutoka Kwa Washindi Hao Mara 12 Wa Ligi Kuu.
Kuondoka Kwake Kunamaanisha Opiyo Na Humphrey Katasi Ndio Makipa Pekee Waandamizi Waliosalia Katika Klabu Hiyo, Na Ingwe Inaweza Kulazimika Kuingia Sokoni Kutafuta Kipa Mpya.
Bonphas Munyasa Alikuwa Akihusishwa Na Uhamisho Wa Kwenda Ingwe, Lakini Mchezaji Huyo Wa Murang’a Seal FC Amechagua Kujiunga Na KCB FC.
Sebastian Wekesa Wa Kariobangi Sharks Ni Chaguo Jingine Kwa Ingwe.
Imetayarishwa na Nelson Andati