NYONGEZA YA MISHAHARA KWA POLISI, MAAFISA WA MAGEREZA WAANZA MWEZI HUU

Rais William Ruto amesisitiza kujitolea kwa serikali kutimiza ahadi yake ya nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa magereza na maafisa wa polisi kuanzia mwezi huu.
Akizungumza Ikulu wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Kamishna Mkuu mpya aliyeteuliwa wa Jeshi la Magereza, Ruto ameapa kuwa serikali yake itatekeleza ahadi yake kwa watumishi hao.
Mwanzoni mwa mwaka, serikali iliapa kwamba maafisa wa polisi na wasimamizi wa gereza wataanza kupokea nyongeza ya mishahara yao ya asilimia 40 kuanzia Julai.
Nyongeza hiyo ya mishahara inalingana na mapendekezo yaliyotolewa na jopokazi lililoongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga mwaka jana.
Imetayarishwa na Janice Marete