#Local News

WAKENYA MAHAKAMANI WAKITAKA RUTO, GACHAGUA NJE

Wakenya 14 wamewasilisha kesi mahakamani wakitaka kuandaliwa kwa kura ya maoni ili kuwaondoa afisini kwa Rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua, wakisema wawili hao wameshindwa kuendesha nchi hasa kutokana na jinsi walivyoshughulikia maandamano.

Kwenye kesi hiyo ambapo Ruto na Gachagua ndio washtakiwa, walalamishi wanahoji kuwa washtakiwa wameshindwa kudhibiti msukosuko wa kisiasa kwa mujibu wa katiba, na badala yake kuwatuma maafisa wa jeshi la KDF dhidi ya waandamanaji wa amani.

Huku wakitaka kura ya maoni iandaliwe kufikia Oktoba mwaka huu, walalamishi wanasema ni ukandamizaji wa haki za kikatiba kuwatumia wanajeshi kuwazuia wakenya kushiriki maandamano ya amani.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAKENYA MAHAKAMANI WAKITAKA RUTO, GACHAGUA NJE

ORODHA YA MAWAZIRI WAPYA

WAKENYA MAHAKAMANI WAKITAKA RUTO, GACHAGUA NJE

AMRI YA RUTO KWA POLISI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *