WACHA MCHANGANYIKO

Mechi ya ufunguzi ya olimpiki ya Sudan kusini iligubikwa na makosa ya aibu ya wimbo wa taifa yaliyofanywa na waandaaji siku ya jumapili.
Timu hiyo ya afrika ya mpira wa vikapu ilionekana kuchanganyikiwa baada ya wimbo wa sudan kuchezwa walipokuwa wakipanga mstari kabla ya mpambano wao na puerto rico.
Mashabiki wa sudan kusini katika uwanja wa stade Pierre-mauroy huko villeneuve-d’ascq walighadhabiki baada ya kusikia wimbo ambao haukuwa wao.
Hitilafu hiyo ilirekebishwa haraka na wimbo sahihi ukachezwa, huku wachezaji na mashabiki wa puerto rico wakipiga makofi kwa pamoja.
Sudan kusini inashiriki mashindano ya mpira wa vikapu ya olimpiki kwa mara ya kwanza na jana wakashinda 90-76 dhidi ya puerto rico.
Utata mwengine ulishuhudiwa pia katika sherehe za ufunguzi ijumaa, wakati timu ya olimpiki ya korea kusini ilipotambulishwa kimakosa kama korea kaskazini.
Imetayarishwa na Janice Marete