DORCAS ODUOR ATEULIWA KUWA MWANASHERIA MKUU
Rais William Ruto amemteua Dorcs Oduor kuwa mwanasheria mkuu ambaye kwa sasa anahudumu kama katibu katika afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ODPP.
Oduor ambaye ni wakili wa mahakama kuu, amewahi kuhudumu kama naibu mkurugenzi katika afisi ya ODPP na mwanasheria wa serikali kwenye afisi hiyo.
Uteuzi wake unajiri baada ya Rebecca Miano ambaye alikuwa amepewa wadhifa huo, kuhamishiwa katika wizara ya utalii.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































