#Football #Sports

MAN U KATIKA NJIA PANDA

Wamiliki wa manchester united wanatarajia kufanya uamuzi wa mwisho iwapo watatumia shilingi bilioni 283 kwa minajili yakupata uwanja mpya wenye viti 100,000 ifikapo mwisho wa 2024.

Mmiliki mwenza wa man united jim ratcliffe anataka kujenga ‘wembley ya kaskazini’ kwa ushirikiano na manispaa ya mji wa trafford, na kwa pamoja wameweka kikosi kazi kutathmini uwezekano wa uwanja mpya na ukarabati wa old trafford.

Kikosi kazi hicho kinaongozwa na lord sebastian coe na kinajumuisha meja mkuu wa manchester andy burnham na nahodha wa zamani wa mashetani wekundu gary neville.

Kikosi kazi tayari kimekutana mara nne, lakini hakuna uamuzi uliotolewa.

Kokubo awakilisha japan

Kipa leo kokubo na kiungo joel chima fujita ndio wachezaji pekee weusi wanaoiwakilisha japan katika soka ya wanaume kwenye olimpiki ya 2024.

Wachezaji wote wawili walizaliwa nchini japan kwa baba wa nigeria na mama wa kijapani.

Wote pia wamesajiliwa katika klabu ya ubelgiji ya sint-truiden

Imetayarishwa na Nelson Andati

MAN U KATIKA NJIA PANDA

BUKEMBE WAZIDI KUONYESHA MAKALI YAO

MAN U KATIKA NJIA PANDA

KUWA MWALIMU NI MWITO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *