KISA CHA KWANZA CHA MPOX CHARIPOTIWA KENYA

Wizara ya afya imegundua kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Mpox ambao husababishwa na virusi vya monkeypox katika kaunti ya Taita Taveta.
Katika taarifa, wizara hiyo imesema mgonjwa wa ugonjwa huo amegunduliwa mpakani alipokuwa akisafiri kutoka Uganda keuelekea Rwanda kupitia hapa nchini.
Wizara hiyo aidha amewatahadharisha wananchi kuwa makini na ugonjwa huo ambao huenezwa kupitia utangamano wa karibu na mwaathiriwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa