#Football #Sports

MATANO APASUA MBARIKA

Robert Matano, kocha mkuu wa zamani wa Tusker FC, amefichua kilichomfanya akaondoka kwa mabingwa hao mara 13 wa Ligi Kuu ya Kenya.

Kuondoka kwake kulihitimisha uhudumu wake wa miaka sita katika klabu hiyo yenye maskani yake Ruaraka, ambapo alishinda mataji matatu yakiwemo ya Ligi Kuu msimu wa 2020-21 na 2021-22 na Kombe la Super Cup 2021-22.

‘Simba’, kama anavyofahamika, alisema aliacha nafasi yake kwa sababu alihisi amefanya mengi kwa klabu na hivyo kuhitaji changamoto mpya.

Hii ilikuwa mara yake ya pili baada ya kuiongoza Tusker kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 2012, na kuweka rekodi ya kocha wa kwanza kubeba mataji matatu ya Ligi akiwa na Tusker.

Matano, ambaye hakufichua mipango yake ya baadaye, amesema misimu mitatu iliyopita ilikuwa migumu zaidi kwake lakini anasema alitumia tajriba yake kukwepa changamoto ili kumaliza kama washindi wa pili kwa Gor Mahia FC.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MATANO APASUA MBARIKA

WINCATE AJIUNGA NA SIMBA QUEENS

MATANO APASUA MBARIKA

SIFAN HASSAN ADHIBITISHA UWEPO WAKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *