#Sports

BUSIA YANAWIRI

Kaunti ya Busia ndiyo mshindi wa mashindano ya shule za upili za wanafunzi walio na mahitaji maalum kse ya eneo la magharibi ambayo yamekamilika katika shule za upili za father okodoi na st. Bridgit kaunti ndogo ya teso ya kati kaunti ya busia.

Kaunti ya Busia imetwaa ubingwa kwenye kandanda na voliboli ya walemavu wavulana, vihiga wakashinda netiboli, taji la voliboli wasichana likatwaliwa na kaunti ya kakamega huku taji la voliboli ya kuketi likitwaliwa na kaunti ya bungoma ambayo pia ilitwaa taji la voliboli ya wanafunzi walio na matatizo ya kuona.

Kaunti ya Kakamega imeshinda michezo ya ndani ikiwemo tenisi ya mezani na badminton kwenye mashindano hayo ya siku tatu yalio ng’oa nanga siku ya jumatatu.

Timu hizo sasa zitabuni timu ya eneo la magharibi ambayo itashiriki mashindano ya kitaifa kaunti ya kisumu mwezi ujao wa nane.

Mwenyekiti wa mashindano hayo eneo la magharibi walter kwanusu akiahidi kuwa watafanya vyema na kutwaa mataji mengi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

BUSIA YANAWIRI

TUBORESHE UTENDEKAZI

BUSIA YANAWIRI

MCHUANO MKALI WA OLYMPIKI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *