RIPOTI YA MAHOJIANO YA MAWAZIRI KUWASILISHWA KESHO
Kamati ya uteuzi ya bunge la kitaifa ikiongozwa na spika wa bunge la kitaifa Moses Masika Wetangula inatarajiwa kuwasilisha ripoti ya mahojiano ya mawaziri hapo kesho, kabla ya vikao vya kujadili ripoti hiyo kufanyika siku ya jumatano wiki hii kuamua hatima ya mawaziri walioteuliwa na rais william Ruto.
Spika wa bunge la kitaifa Moses Masika Wetangula amewahakikishia wakenya kuwa vigezo vya uadilifu ,sheria na tajriba ya kikazi ndivyo vitakavyozingatiwa zaidi katika ripoti hiyo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































