KENYA YAANZA KUWAHAMISHA RAIA WAKE KUTOKA LEBANON

Kenya imeungana na nchi zinazowataka raia wake kuondoka Lebanon, huku hali ya wasiwasi ikizidi kuzua hofu ya kuenea kwa migogoro katika nchi za Mashariki ya Kati.
Eneo la Mashariki ya Kati linakumbwa na mvutano mkubwa baada ya Iran kuapa kulipiza kisasi kwa Israel kutokana na mauaji ya Ismail Haniyeh, kiongozi wa kundi la Hamas.
Sasa, wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Kenya kupitia Idara ya Masuala ya Diaspora imewataka raia wake wanaoishi Lebanon kuondoka nchini au kuhamia maeneo salama.
Imetayarishwa na Janice Marete