“MAANDAMANO KAME” NCHINI

Hali ya utulivu imeshuhudiwa katika sehemu mbali mbali nchini licha ya vijana wa Gen Z kutangaza kufanya maandamano waliyoytaja kuwa makubwa zaidi yaliyopewa jina la Nane nane hii leo.
Hata hivyo katika miji mbali mbali ikiwemo Nairobi na Kisumu, biashara nyingi zimesalia kufungwa, wafanyabiashara wakihofia kuporwa na wahuni.
Mjini Kisumu, vijana wamesema kwamba hawajarishishwa na mikakati ya Rais William Ruto, wakiapa kuendelea na maandamano.
Aidha, wahudumu wa biashara jijini humo wamewataka vijana kusitisha maandamano.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa