MAKATIBU 19 WA BARAZA LA MAWAZIRI WAMEAPISHWA KATIKA IKULU YA NAIROBI

Makatibu 19 wa Baraza la Mawaziri walioteuliwa na Rais William Ruto wameapishwa kama sehemu ya serikali pana.
Rais Ruto ametangaza rasmi uteuzi wa Mawaziri 19 katika nyadhifa zao kulingana na Kifungu cha 152 (2) cha Katiba ambacho kinampa mkuu wa nchi mamlaka ya kuteua na kuwatangaza Mawaziri hao baada ya kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa.
Kamati ya Bunge ya Kitaifa kuhusu Uteuzi ilifanya zoezi la uhakiki wa siku nne ili kubaini iwapo Mawaziri hao wanafaa kushikilia nyadhifa hizo.
Imetayarishwa na Janice Marete