SERIKALI YA KISUMU YATAKIWA KUFANYA KIPAUMBELE MASWALA YA AFYA
Washikadau katika sekta ya afya ya umma katika kaunti ya Kisumu wametoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo kufanya kipaumbele swala la afya ya umma kuhakikisha kwamba mikakati maalumu imewekwa kuimarisha miundomsingi na vile vile kuhakikisha kwamba wahudumu wa afya wa kutosha wanaajiriwa.
Aidha wanamtaka gavana Anyang Nyongo kuhakikisha idara ya afya ya umma inatengewa fedha za kutosha ili kufanikisha utekelezwaji wa shughuli mbali mbali za idara hiyo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































