#Local News

SIFUNA, NASSIR KUWA MANAIBU WA RAILA KATIKA MAPENDEKEZO YA MABADILIKO YA ODM

Seneta wa kaunti ya nairobi Nairobi ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna na Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sheriff Nassir wanatazamiwa kutwaa uongozi wa chama cha ODM iwapo mgombea wa Raila Odinga wa AUC atafanikiwa.

Safu hiyo ni sehemu ya pendekezo la vigogo wa ndani wa chama wenye nia ya kuhakikisha mabadiliko yanafanyika, kufuatia kuchaguliwa kwa vinara wa chama hicho Ali Hassan Joho na Wycliffe Oparanya katika serikali.

Wawili hao wanatazamiwa kuchukua wadhifa wa naibu viongozi wa chama katika mabadiliko ambayo yanatarajiwa kutekelezwa wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Usimamizi cha leo Ijumaa.

Mkutano huo utaongozwa na kinara wa Upinzani Raila Odinga.

Imetayarishwa na Janice Marete

SIFUNA, NASSIR KUWA MANAIBU WA RAILA KATIKA MAPENDEKEZO YA MABADILIKO YA ODM

GAVANA MWANGAZA AZIMIWA, TENA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *