DHULUMA KIMYA KIMYA BUSIA

Mkurugenzi wa shirika moja la kijamii katika kaunti ya Busia Mary Makokha, amewahimiza wakazi wa kaunti hiyo kujitokeza na kuzungumzia ongezeko la visa vya duluma za kingoni ili kuifanya Kaunti hiyo kuwa eneo salama la kuishi.
Kwa mjibu Makokha, Kaunti ya Busia inashudia visa vingi vya unajisi na ubakaji, kuanzia miongoni mwa Watoto walio chini ya mwaka mmoja hadi hadi akina mama walio na zaidi ya miaka 80, suala analosema linahitaji juhudu za pamoja kulikabili.
Wakati uo huo, Makokha amevitaka vitengo vya uchunguzi kuhakikisha ushahihidi na mashahidi katika kesi zinazohusiana na uovu huwa wanalindwa ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa