HATUA ZA MUTUA KUEPUSHA MGOMO

Waziri wa leba Alfred Mutua amefanya kikao na viongozi wa chama cha kitaifa cha kutetea maslahi ya walimu KNUT kwa lengo la kujadili utekelezwaji wa mkataba wa maelewano wa mwaka 2021 ili kuepusha mgomo unaonukia wa walimu.
Mutua amesema kwamba mkutano huo umelenga kupata mnwafaka kuhusu matakwa ya walimu ili kuzuia mgomo uliotangazwa na chama cha KNUT.
Hapo jana, katibu mkuu wa KNUT Collins Oyuu alitangaza kwamba katu wanachama wake hawatarejea kazini muhula wa ujao iwapo matakwa yao hayatatekelezwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa