MAKARIBISHO MAALUMU

Kikosi cha wanaradha wa Kenya kilichoshiriki olimpiki ya mwkaa huu jijini paris kimeondoka leo alfajiri kwa ndege maalum uwanja wa JKIA kuelekea mjini Eldoret kwa dhifa maalum ya kiamsha kinywa katika ikulu ya rais William Ruto mjini humo.
Waziri wa michezo kipchumba murkomen na katibu Peter Tum pia nao wameelekea eldoret wakitokea uwanja wa ndege za kijeshi wa kahawa garrison pamoja na wanariadha wengine.
Huu ni mualiko maalum kutoka kwa rais kuwapokea na kuwashukuru wanariadha hao ambao pia watakuwa wanarudisha bendera waliopokezwa kwenda nayo Paris.
Imetayarishwa na Nelson Andati