WANAWAKE WANAHIMIZWA KUWANIA UONGOZI

Afisa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC Marijan Hussein Marijan amewahimiza wanawake haswa walio na ulemavu kujitokeza na kuwania nyathifa mbali mbali za uongozi kwani katiba inawaruhusu kufanya hivyo.
Marijan amesema kuwa tume ya IEBC imeweka mikakati ya kuwahamasisha wanawake haswa walio na ulemavu kuwania nyathifa mbali mbali za uongozi.
Imetayarishwa na Janice Marete