HATO APATIKANA

Baada ya simu ya Jane Hato wa Kenya Police Bullets kuzimwa aliporipotiwa kutoweka hapo jana alipokuwa akitoka nyumbani kuelekea eneo la GSU kukutana na wanasoka wenzake kwa safari ya kuelekea nchini Ethiopia kwa mashindano ya Cecafa, ufuatiliaji wa maongezi na mawimbi ya simu (Phone Tracking) ulionyesha sehemu ya Juja kama eneo alilo.
Kwa msaada wa idara ya ujasusi (DCI), mawimbi ya simu yake ya rununu yamefuatiliwa hadi aliko huko Juja alipopatikana akiwa salam salmin, ameeleza mamake mzazi Ann Aluoch ambaye pia ni naibu kocha wa Junior Starlets.
Maafisa wa polisi kwa sasa wanaendelea na harakati za kumkomboa msichana huyo. Taarifa zaidi zitajiri kwa mujibu wa tukio.
Imetayarishwa na Nelson Andati