#Local News

IPOA KIKAANGANI MBELE YA BUNGE

Mamlaka ya kuchunguza utendakazi wa polisi IPOA imejipata pabaya baada ya kamati ya uangalizi na utekelezwaji wa sheria katika bunge la kitaifa kutilia shaka uwezo wake wa kutekeleza majukumu yake, hasa kushindwa kuwawajibisha maafisa wa polisi waliokiuka sheria wakati wa kuwakabili waandamanaji.

Kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake Gathoni Wamuchomba imeibua hofu kuhusiana na kushindwa kwa mamlaka hiyo kuhainisha idara za polisi wa utawala na wale wa kawaida katika idara ya polisi, na ongezeko la ripoti za polisi kushambuliwa na umma.

Hata hivyo, afisa mkuu mtendaji wa IPOA Elema Halake, amesema kwamba ana matumaini kuwa idara ya polisi inafuata amri ya mahakama kuu ya kuwataka polisi kujitambulisha wanapokuwa kazini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

IPOA KIKAANGANI MBELE YA BUNGE

WANJIGI AENDELEA ‘KULINDWA’ NA MAHAKAMA

IPOA KIKAANGANI MBELE YA BUNGE

WAZIRI WA KILIMO AZURU GHALA ZA MAJANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *