RUTO AAHIDI POSHO LA WASANII

Rais William Ruto amesema kwamba serikali inatambua umuhimu wa uvumbuzi na ubunifu katika kubuni nafasi za ajira nchini, na kusema kwamba serikali imejitolea kuhakikisha kwamba wanamuziki na wasanii wanafaidika kutokana na kazi yao.
Rais ameyasema haya katika ikulu ndogo jijini Eldoret alipokuwa akitumbuizwa na washindi wa tamasha za muziki.
Wakati uo huo, Rais amemwagiza Waziri wa michezo kipchumba Murkomen kuhakikisha wasanii wanafaidika kutokana na usanii wao, huku naibu wake Rigathi gachagua akiwapongeza washindi kwa viwango vyao vya ubunifu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa