#Football #Sports

TOTTE YAMSIMAMISHA BISSOUMA

Tottenham imemsimamisha Yves Bissouma kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Leicester City siku ya Jumatatu baada ya picha kuonekana kuonyesha kiungo huyo akivuta kiko cha ‘Shisha’.

Spurs wamechukua hatua hiyo licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kuomba msamaha kwa kile alichokiita kutokuwa na uamuzi sahihi, baada ya kuchapisha video yake kwenye mitandao ya kijamii Jumamosi ambayo ilionyesha akivuta kiko akiwa varandani.

Shisha ina gesi ya nitrous oxide – pia inajulikana kama gesi ya kucheka kwa matumizi ya burudani na ivutaji wake umekuwa kosa la jinai nchini Uingereza tangu 2023 na kunaweza kusababisha kifungo cha miaka miwili jela.

Bissouma alicheza kwa dakika 45 katika kichapo cha Spurs katika mechi ya kirafiki dhidi ya Bayern Munich Jumamosi mchana, kabla ya kuchapisha video hiyo.

Imetayarishwa na Nelson Andati

TOTTE YAMSIMAMISHA BISSOUMA

SANDRO TONALI YUPO ANGEE

TOTTE YAMSIMAMISHA BISSOUMA

WAZIRI WA ZAMANI BETT, WENGINE WATATU WAJERUHIWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *