#Local News

AMUUA MKEWE NA KISHA AKATOROKA

Polisi wanamsaka mwanaume mmoja huko Kimilili Kaunti ya Bungoma , mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanamke mwenye umri wa miaka 23 ambaye ametambulika kwa jina Belinda Wanjala.

Mshukiwa huyo anaaminika kuwa mumewe marehemu ambaye walikuwa wanaishi katika chumba ulikopatikana mwili wa marehemu.

Mwili wa Belinda umepatikana ukiwa kwenye dimbwi la damu ndani ya nyumba yake ukiwa na majeraha makubwa kichwani, miguuni na mikononi.

Sababu ya mauaji hayo bado haijajulikana, mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi.

Imetayarishwa na Janice Marete

AMUUA MKEWE NA KISHA AKATOROKA

HATIMA YA GAVANA MWANGAZA YAANZA KUJADILIWA NA

AMUUA MKEWE NA KISHA AKATOROKA

KENYA POLICE WASHINDWA KUFYATUA RISASI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *