#Football #Sports

GOR MAHIA WALAMBISHWA VUMBI

Bao pekee lililofungwa dakika ya 64 na Mohammed Mussa wa Al Merrikh Benteu ya Sudan Kusini liliizamisha Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya awali ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mechi hiyo ilichezwa jana jioni kwenye Uwanja wa Juba, Sudan ya Kusini ni muendelezo wa mabingwa hao wa Kenya kuwa na matokeo mabaya tangu ibebe taji la Ligi Kuu msimu uliopita.

Timu hiyo ilifanya vibaya katika michuano ya Kombe la Kagame 2024 iliyochezwa jijini Dar es Salaam mwezi uliopita.

Katika michuano ya Kagame Gor iling’olewa makundini kwa kufungwa mechi mbili dhidi ya Al Hilal ya Sudan na waliobeba ubingwa, Red Arrows ya Zambia na kuambulia sare y 1-1 dhidi ya ASAS ya Dijbouti.

Kwa kipigo hicho K’Ogalo sasa inahitaji ushindi kuanzia mabao 2-0 katika mechi ya marudiano Jumapili ijayo, hapa jijini Nairobi ili itinge raundi ya pili.

Imetayarishwa na Nelson Andati

GOR MAHIA WALAMBISHWA VUMBI

KENYA POLICE WASHINDWA KUFYATUA RISASI

GOR MAHIA WALAMBISHWA VUMBI

KABRAS RFC WABEBA KIKOMBE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *