#Football #Sports

KENYA BULLETS WAANZA KWA SARE

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Kenya (KWPL) Kenya Police Bullets walifungua kampeni yao ya CECAFA kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Yei Joint Stars.

Timu ya Bullets inayoongozwa na Beldine Odemba inashiriki kwa mara ya kwanza katika ulingo wa bara, ikishiriki mechi za Kanda za CECAFA za kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya CAF ya Wanawake inayoendelea Addis Ababa, Ethiopia.

Awali, timu hiyo ilipangwa kucheza na Warriors Queens ya Zanzibar katika mchezo wa kwanza wa Kundi A Jumamosi, lakini mpinzani huyo alijiondoa kwenye michuano hiyo, hivyo kulazimika kupangwa upya.

Bullets inalenga kuwa timu ya pili ya Kenya kufuzu baada ya Vihiga Queens, ambao walijinyakulia tiketi yao 2021 wakati mchujo ulipoandaliwa jijini Nairobi.

Bullets watacheza mechi yao ijayo dhidi ya CBE Women FC Jumatano, Agosti 21 wakitarajia kusajili ushindi wao wa kwanza na kujipa nafasi ya kufuzu kwa nusu fainali

Imetayarishwa na Nelson Andati

KENYA BULLETS WAANZA KWA SARE

AFARIKI KWA DAU YA MIA TATU HUKO

KENYA BULLETS WAANZA KWA SARE

SARAH MORAA ATARAJIA KUBEBA TAJI.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *