KENYA POLICE WASHINDWA KUFYATUA RISASI

Kenya Police ilishindwa kuchukua faida ya nyumbani katika mechi ya mkondo wa kwanza ya Kombe la Shirikisho la CAF baada ya kutoka sare tasa na Ethiopia Coffee kwenye Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo.
Polisi, ambao walikuwa wanashiriki kwa mara ya kwanza kwenye shindano hili, walikuwa wamepigia upato zaidi katika mchezo huu kutokana na kwamba walikuwa wakicheza mbele ya mashabiki wao, lakini waliishia kushika tama.
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa timu hizo mbili sasa zitamenyana kuwania kufuzu katika raundi ya pili ya hatua ya awali, inayotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia wikendi ijayo.
Imetayarishwa na Nelson Andati