BADO HATUJAANZA MAZOEZI MUHAMBE ASEMA

Kocha Wa Klabu Ya Madira Soccer Assassins Francis Muhambe, Anasema Hawaja Anza Mazoezi Kama Ilivyo Pangwa Kwa Kuwa Wamekumbwa Na Matatizo Ya Kifedha.
Muhambe Anasema Pesa Walio Ahidiwa Na Kaunti Ya Vihiga Bado Hawajaipata Ili Kusaidia Matayarisho Yao Kushiriki Ligi Ya Daraja La Pili Kwa Wanawake Msimu Ujao.
Muhambe Vilevile Ameweka Wazi Kuwa Nelly Achieng Amejiunga Na Klabu Ya Fountain Gate Ya Tanzania Naye Charity Midewa Amejiunga Na Klabu Ya Rayon Sports Nchini Rwanda.
Hata Hivyo Kocha Huyo Anasema Kwa Upande Wao Mpaka Sasa Hawaja Sajili Wachezaji Wapya
Msimu Uliopita Madira Walishushwa Daraja Kutoka Ligi Kuu Ya Wanawake Nchini Hadi Ligi Ya Nsl .
Imetayarishwa na Nelson Andati