DCI YATANGAZA ZAWADI KUHUSIANA NA KHALISIA

Huku msako dhidi ya mshukiwa mkuu wa mauaji ya Kware Collins Khalisia na raia wa kigeni ukiendelea, idara ya upelelezi DCI imetangaza kutoa zawadi kwa yeyote atayetoa taarifa kuhusiana na aliko mshukiwa huyo.
Katika taarifa kwa umma, DCI imesema itatoa ilichotaja kama zawadi nzuri kwa atakayesadia kumkamata Khalusia aliyetoroka majuzi kutoka kituo cha polisi cha Gigiri.
Kwa mujibu wa idara hiyo, aliye na taarifa anaweza kutoa taarifa hizo kwa njia ya siri kwa kupiga nambari za polisi au kuripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu naye.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa