#Football #Sports

TUNAREJEA KWA KISHINDO

Bayer Leverkusen wameapa kufanya mambo makubwa tena msimu huu baada ya kushinda makombe mawili msimu jana ikiwemo taji la Bundesliga.

Leverkusen wataanza msimu dhidi ya Borussia Moenchengladbach kesho, huku meneja Xabi Alonso akisema kuwa timu yake ina uwezo wa kutetea mataji yake.

Mshambulizi wa Leverkusen, Nathan Tella pia ameiunga mkono timu yake kwa msimu mwingine mzuri, licha ya wapinzani wao wakuu Bayern Munich kutumia pesa nyingi katika dirisha la usajili la sasa.

Msimu uliopita Leverkusen walishinda ligi kuu kwa mara yao ya kwanza, na changamoto ni kudhibitisha kwamba hawakushinda kibahati.

Imetayarishwa na Nelson Andati

TUNAREJEA KWA KISHINDO

KALULU AJIUNGA NA JUVENTUS

TUNAREJEA KWA KISHINDO

MTIHANI BADO UPO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *