MWANAMKE AMCHOMA KISU NA KUMUUA MUMEWE HUKO KASARAN NAIROBI

Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya kudaiwa kumuua mumewe katika vita vinavyoshukiwa kuwa vya nyumbani huko Kasarani,kaunti ya Nairobi.
Imebainika kuwa wanandoa hao walikuwa wamezozana na kupigana kabla ya mwanamume huyo kudungwa kisu kifuani.
Kulingana na polisi, mwanamke huyo alitumia kisu cha jikoni kumchoma mwanamume huyo na kumuua papo hapo.
Mwanamke huyo amekamatwa baadaye na kueleza kuwa alikuwa akijilinda kutokana na kushambuliwa na mumewe.
Mwili huo umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi.
Imetayarishwa na Janice Marete