KUPPET YASAMBARATISHA MASOMO BUNGOMA

Viongozi wa chama cha KUPPET kaunti ya Bungoma wamesambaratisha shughulli za masomo katika shule mbalimbali ikiwemo ile ya kitaifa ya wasichana ya Lugulu kwenye kaunti hiyo baada ya kuwafurusha walimu waliokuwa wakiendeleza shughuli za masomo.
Wakiongozwa na katibu wa chama hicho kaunti ya Bungoma Augustine Luketero, wamesema kuwa hawataraejea madarasani hadi serikali itakaposhughulikia maslahi yao huku wakitishia kuwachukulia hatua walimu watakaokiuka agizo la mgomo.
Hata hivyo, wazazi wakiongozwa na John Wanyama wameikosoa serikali kwa kushindwa kusaka suluhu kwa mgomo huo, na kuilaumu KUPPET kutokana na hatua yao ya kuvamia shule.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa