BRENTFORD IMEMSAJILI MSHAMBULIAJI WA BRAZIL NUNES KUTOKA GREMIO

Brentford imemsajili winga wa Brazil Gustavo Nunes kutoka klabu ya Gremio ya Brazil Serie A, kwa ada ya zaidi ya pauni milioni 10
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 amesaini mkataba wa miaka sita, na klabu hiyo ina chaguo la kuongeza mkataba huo kwa miaka miwili
Nunes alijiunga na akademia ya vijana ya Gremio mnamo 2021 na akacheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza mnamo Februari 2024.
Aliichezea Gremio mechi 20 katika ligi kuu ya Brazil msimu huu, akifunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya mabao.
Imetayarishwa na Janice Marete