LENOLKULAL ROHO MKONONI HUKUMU IKINUKIA

Gavana wa zamana wa Samburu Moses Lenolkalal anatarajiwa kufahamu hukumu yake muda wowote kuanzia sasa baada ya mahakama inayosikiliza kesi za ufisadi hapo jana kumpata na hatia ya ufisadi unaohusisha shilingi milioni 84.
Lenolkulal ambaye alishtakiwa na wenzake 10 ambao pia wamepatikana na hatia, ameiomba mahakama kumpa kifungo cha nyumbani au faini na wala si cha gerezani.
Hata hivyo, wakenya wanasubiri kwa hamu kuona iwapo hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Thomas Nzioki atakubali ombi hilo au atamhukumu kifungo cha gerezani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa