NINAONDOKA KWENYE WIZARA YA AFYA NIKIWA NA FURAHA SANA – NAKHUMICHA

Aliyekuwa Waziri wa Afya Susan Nakhumicha leo amekabidhi hati hiyo kwa mrithi wake Deborah Mulongo, aliyeingia madarakani Agosti 8, 2024.
Wakati wa makabidhiano hayo katika Afya House, Nakhumicha amesema kwamba anaondoka kwenye hati yake akiwa ametekeleza mageuzi ya kuimarisha sekta ya afya nchini Kenya.
Miongoni mwa mageuzi ambayo waziri huyo wa zamani anajivunia ni kuanzishwa kwa Wakuzaji Afya ya Jamii, ambapo zaidi ya wataalamu 100, 000 wamepewa mafunzo ya kutoa huduma za kimsingi za matibabu.
Imetayarishwa na Janice Marete