MOTO WATEKETEZA MAKTABA BUNGOMA HIGH

Mali yenye thamani isiyojulikana imeteketea katika shule ya upili ya wavulana ya Bungoma iliyoko mjini Bungoma mapema leo huku chanzo cha moto kikiwa bado hakijabainika.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Enoch Andanje, moto huo uliogunduliwa mwendo wa saa kumi na mbili na nusu asubuhi umesababisha wanafunzi kupoteza bidhaa zao ikiwemo malazi, na kuongeza kuwa ni wanafunzi wa kidato cha nne pekee ndio waliokuwa shuleni.
Naye Clabaton Muchanga ambaye ni mzazi na jirani wa shule hiyo ameilaumu idara ya wazima moto katika kaunti ya Bungoma kwa madai ya kuzembea na kusababisha uharibifu mkubwa shuleni humo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa