WAFANYAKAZI WA ANGA KATIKA JKIA WAANDAMANA

Wafanyakazi wa usafiri wa anga chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (KAA) wamefanya maandamano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).
Wakiwa na mabango, wafanyakazi hao wamelaani ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ambao utaipa kampuni ya Adani Group Holdings yenye makao yake makuu nchini India mamlaka ya kuchukua shughuli katika uwanja wa ndege unaoongoza Afrika Mashariki.
Wafanyakazi wa KAA wanahoji kuwa mkataba wa Adani unahatarisha kazi zao kwa ajili ya wafanyakazi wa kigeni.
Imetayarishwa na Janice Marete