TUEKEZE ZAIDI

Mshindi mpya wa medali ya fedha katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu Samson Ojuka ametoa wito wa kuwekeza zaidi katika mashindano hayo ikiwa Kenya inataka kupelekana sako kwa bako na miamba wa dunia.
Ojuka alishinda medali ya fedha katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Paris mnamo Jumanne katika fainali yaurukaji kwa urefu kitengo cha T37 kwa wanaume, akiruka umbali wa mita 6.20 katika jaribio la nne, na kuweka rekodi mpya ya afrika.
Ojuka, mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa sheria katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, ana ndoto kubwa baada ya mafanikio makubwa ya Paris ambayo yalimfanya kushinda medali ya kwanza iliyokuwa ikisubiriwa na Kenya, na sasa anakodolea macho rekodi ya dunia.
Ojuka alirejea nchini mapema leo.
Imetayarishwa na Nelson Andati