KAIMU INSPEKTA WA POLISI GILBERT MASENGELI APUUZA WITO WA MAHAKAMA TENA
Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli kwa mara ya sita amefutilia mbali wito uliotolewa na Mahakama Kuu kumtaka afikishwe mahakamani kujibu maswali ya waliko watu watatu waliopotea mtaani Kitengela kaunti a kiambu.
Timu yake ya wanasheria ilimweleza Jaji Lawrence Mugambi kwamba kwa sasa anajishughulisha na masuala ya usalama kaunti ya Wajir.
Naibu Inspekta Jenerali wa Huduma ya Polisi ya Kenya Eliud Lagat amefika mahakamani kwa niaba yake.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































