RUTO AENDELEA KUAHIDI NYUMBA

Rais William Ruto ameahidi kuwa serikali yake itawajengea nyumba 40,000 chini ya mpango wa makazi ya bei nafuu wakazi wa Nairobi waliopoteza makazi yao kufuatia mafuriko.
Akizungumza mtaani Kibra ambako amezuru kukagua ujenzi wa mradi huo, Ruto amesema kandarasi ya ujenzi wa makazi hayo itatolewa hivi karibuni kwa lengo la kuhakikisha watu waliohamishwa na serikali kutokana na mafuriko wanapata makazi.
Aidha, amesema kwamba kuna zaidi ya nyumba 110,000 kote nchini ambazo zinaendelea kujengwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa