VIONGOZI KUTOKA KAUNTI 3 WAMWIDHINISHA KINDIKI KUWA KIGOGO

Viongozi kutoka kaunti za Tharaka Nithi, Embu na Meru wakiwemo wabunge na maseneta wamemwidhinisha Waziri wa usalama wa kitaifa Profesa Kithure Kindiki kuwa kigogo wao, wakimpa majukumu ya kuwaunganisha na serikali tendaji.
Viongozi hao wameafikia uamuzi wao baada ya kongamano la wajumbe kutoka mashariki mwa Mlima Kenya mjini Embu.
Wamekutana kwa lengo la kujadili mustakabali wa eneo hilo kiuchumi na ajenda yao ya kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa