SERIKALI MBIONI KUIMARISHA AFYA YA AKILI
Visa vya matatizo ya afya ya akili vinatarajiwa kupungua baada ya wizara ya afya kuzindua mwongozo wa kwanza wa kliniki kwa lengo la kudhibiti visa hivyo kwa kuimarisha upimaji na matibabu kwa waathiriwa.
Mkuu wa idara ya afya ya familia Bashir Isaak amesema mwongozo huo unalenga kushughulikia mwanya wa asilimia 75 katika huduma za kimatibabu uliopo kwa sasa huku visa hivyo vikiongezeka.
Mwongozo huo unalenga kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya kuhusiana na namna ya kukabiliana na matatizo ya afya ya akili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































