WASHUKIWA WAWILI WA KESI YA MAUAJI YA SIAYA KUWA MASHAHIDI WA SERIKALI
Jean Ogol, mwalimu wa shule ya msingi na Henry Opiyo, waliokamatwa kuhusiana na mauaji ya mzee wa miaka 40 huko Bondo, Kaunti ya Siaya hawatakabiliwa na mashtaka ya mauaji tena na badala yake watakuwa mashahidi wa serikali katika kesi hiyo ya mauaji ambapo washukiwa wakuu bado wanazuiliwa.
Wawili hao walikamatwa mnamo Agosti 11, 2024 kufuatia kifo cha Marwara, ambaye mwili wake ulipatikana ukining’inia katika nyumba ambayo haijakamilika ya Ogol katika lokesheni ndogo ya Bar Kowino.
Hakimu Mkuu Ogoti aliamuru kuwa dhamana ya pesa taslimu ya shilingi 300,000 ambayo awali ilikuwa imetolewa kwa Ogol na Opiyo irudishwe kwa wawili hao kufuatia maombi ya wakili wao Dola Indidis.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































