SINA HARAKA KUINGIA MARATHON

Bingwa wa Olimpiki mara mbili Beatrice Chebet anasema hana haraka ya kuhamia mbio za marathon lakini badala yake atatumia mbinu za taratibu kuhamia mbio za barabarani.
Mshikilizi huyo wa rekodi ya dunia ya mbio za mita 10,000 ana nia ya kufuata nyayo za bingwa wa Boston Marathon Hellen Obiri na mshindi wa London Marathon 2023 Sifan Hassan, ambao wote walifanya mabadiliko yao kwa mafanikio.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa na msimu mzuri, akipata ushindi wa kihistoria mbio za mita 5000 na 10,000 katika
Olimpiki ya Paris na rekodi ya dunia ya mita 10,000.
Pia alishusha rekodi ya dunia ya mbio za barabarani za 5km alipotumia dakika 14:13 mjini Barcelona mwishoni mwa mwaka jana.
Imetayarishwa na Nelson Andati