OLUNGA ASHINIKIZWA KUREJEA KWENYE KIKOSI CHA HARAMBEE STARS

Kiungo wa kati wa harambee stars Richard Odada anatumai nahodha wa stars Michael Olunga atashiriki mechi ijayo ya kufuzu dimba la AFCON 2025 dhidi ya kenya na Cameroon mwezi Oktoba.
Olunga amekosa mechi mbili za mwisho za kufuzu dhidi ya Zimbabwe na Cameroon, huku Odada akikiri walikosa uongozi wa Olunga, na makali ya kufunga mabao mengi.
Kenya ilifunga namibia 2-1 jumanne wiki hii na kuvuka kileleni mwa kundi J kwa pointi nne baada ya kutoka sare dhidi ya zimbabwe katika mechi ya awali.
Kenya imeratibiwa kucheza na Cameroon mara mbili tarehe 7 na tarehe 15 mwezi ujao, na katika mechi hizo mbili mshindi wa kundi hilo atajulikana.
Timu mbili za kwanza katika kila kundi zitafuzu kwa mashindano ya afcon 2025 kule yatakayoandaliwa nchini Morocco.
Mara ya mwisho kwa kenya kufuzu dimba la AFCON ilikuwa 2019 kule misri.
Imetayarishwa na Osoro Kennedy