UTULIVU WAREJEA MARIKITI, VIUNGA VYAKE

Utulivu umerejea kwenye maeneo yaliyo karibu na soko la wakulima katika barabara ya Haile Selassie jijini Nairobi ambapo kimeshuhudiwa mapema leo kufuatia makabiliano baina ya maafisa wa polisi na wafanyabiashara ambao wanapinga kuhamishwa kutoka soko hilo.
Kwa zaidi ya kipindi cha saa 5 polisi na askari wa kaunti wamekuwa wakiwakabili wafanyabiashara hao kwa vitoza machozi na kulemaza shughuli katikati mwa jiji la Nairobi.
Wafanyabiashara hao wamewasha magurudumu kwenye barabara kadhaa kulalamikia mpango wa serikali ya kaunti kuwahamishia kwenye soko jipya liliko katika barabara ya Kangundo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa