WATU WANNE WAKAMATWA KUFUATIA WIZI WA PIKIPIKI HUKO TRANSNZOIA

Watu wanne wamekamatwa eneo la Kiminini katika kaunti ya Transnzoia kufuatia wizi wa Piki piki zaidi ya 60.
Maafisa wa polisi katika kaunti ya Transnzoia kwa ushirikiano na wenzao wa kaunti ya Uasin Gishu wamefanikiwa kupata pikipiki hizo ambazo zinaaminika kuibiwa katika wizi wa kimabavu uliosababisha vifo vya watu watano.
Wakaazi wamewapongeza maafisa wa polisi kwa kufanya oparisheni hiyo ambayo wanasema kuwa itaimarisha usalama wao.
Imetayarishwa na Janice Marete