GOR MAHIA KUGARAGAZANA NA YANGA SC YA TANZANIA JANUARI, 2025 KWENYE UGA WA SIAYA
Gor Mahia sasa watamenyana na Yanga SC ya Tanzania siku ya kuzindua uga wa Siaya miezi mitatu zijazo.
Hii ni kwa mujibu wa gavana wa kaunti ya Siaya James Orengo kupitia ukurasa wake wa X, maarufu Twitter. Gavana huyo alidokeza amefanya mazungumzo na rais wa klabu ya Yanga SC Hersi Said na kufikia makubaliano.
Mechi kati ya mabingwa wa Kenya Gor Mahia na miamba wa soka nchini Tanzania Yanga, itachezwa mnamo tarehe 1 Januari, 2025 katika uwanja mpya wa Siaya.
Hii itakuwa mechi ya uzinduzi wa uwanja wa Siaya ambayo imekuwa ikikarabatiwa kufikia viwango vya mikataifa.
Rais wa Yanga amekuwa nchini Kenya kushiriki mkutano wa CAF, ulioshuhudiwa pia na Rais wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe.
Ujio wa Motsepe nchini ni katika uhakiki wa matayarisho ya Kenya kuandaa mashindano ya CHAN ya waka 2025 pamoja na maandalizi ya AFCON 2027 kwa ushirikiano na Uganda na Tanzania.
Awali, Orengo na mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier walisafiri Tanzania na kukutana na rais wa Yanga na kujadili uwezekano wa Yanga kucheza na Gor Mahia siku ya ufunguzi wa uwanja huo.
Imetayarishwa na Kennedy Osoro
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































