MATOKEO YA DIMBA LA KLABU BINGWA BARANI ULAYA

Timu ya Bayern Munich iliicharaza Dynamo Zagreb mabao 9-0 katika uga wao wa nyumbani- Allianz Arena.
Kwenye mechi hiyo ya kukata na shoka, Harry Kane alifunga mabao matano huku Leroy Sane, Michael Olise, Raphael Guerreiro na Leon Goretzka wakifunga bao moja kwa kila mmoja.
Mabingwa watetezi Real Madrid walifunga VfB Stuttgart mabao 3-1 na kufufua matumaini yao ya kutetea taji hilo msimu huu.
Timu ya uingereza ya Liverpool iliicharaza Milan mabao 3-1 huku Juventus ikipata ushindi wa 3-1 dhidi ya PSV.
Leo saa nne usiku, PSG watagarazana na Girona, Manchester City waialike Inter Millan, kisha Club Brugge wawakaribishe wana Dortmund ambao walifika kwenye fainali msimu uliopita dhidi ya Mabingwa watetezi Real Madrid.
Imetayarishwa na Kennedy Osoro